[Latest Updates]: Mbogwe Yawa Mfano Sekta ya Madini

Tarehe : June 9, 2025, 10:40 a.m.
left

Yafikia asilimia 70 ya makusanyo.

Yaweka mikakati thabiti kufikia malengo yajayo.

Yaendelea kusimamia miradi ya kimkakati.

Mbogwe-Geita

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameupongeza Mkoa wa Kimadini wa Mbogwe kwa kazi nzuri inayofanya ikiwa ni pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali madini ambapo kufikia mwaka 2024, Sekta ya Madini imefanikiwa kuchangia  asilimia 10 katika Pato la Taifa.

Dkt. Kiruswa alitoa pongezi hizo akiwa katika ziara maalamu Wilayani Mbogwe ambapo  alipokea  taarifa ya maendeleo ya Sekta ya Madini katika mkoa wa kimadini wa Mbogwe iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed.

Dkt. Kiruswa aliwasisitiza watendaji wa Ofisi ya Madini Mbogwe kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali waliopo katika mnyororo wa thamani madini ili kuendelea kuifungamanisha Sekta ya Madini na sekta nyingine kiuchumi.

Awali , Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed alieleza kwamba, kutokana na  jitihada mbalimbali  zinazofanywa na  Mkoa wa kimadini wa Mbogwe zimepelekea kufikia asilimia 70 ya makusanyo ya maduhuli kwa kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Juni 2025.

Akielezea kuhusu mipango endelevu iliyowekwa ili kuhakikisha  Sekta ya Madini inaendelea kutoa mchango mkubwa kwa wilaya na taifa kwa ujumla, Sakina alibainisha kuwa, mpaka sasa zaidi ya vitalu  5000 vya madini  vimetolewa kwa wananchi kwa lengo la kushirikisha wananchi katika  kuendeleza uchimbaji ili kuongeza tija ya uchumi kwa ngazi ya wilaya na taifa.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Mbogwe Mhandisi Jeremiah Hango alitabaibisha mikakati mbalimbali iliyowekwa na mkoa ikiwa pamoja na kufuatilia kwa ukaribu migodi iliyosimama kwa muda  mrefu ili kubaini changamoto husika na kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali.

Mkakati mwingine ni kusimamia na kufuatilia  kwa ukaribu  miradi ya ujenzi wa miundombinu ya serikali na sekta binafsi ikiwemo miradi ya ujenzi wa barabara inayotekelezwa na wakandarasi ili kukusanya  maduhuli yatokanayo na madini ujenzi.

Pia, kuendelea kutoa huduma za haraka  pamoja na ushauri wa kitaalam wadau wote waliowekeza katika miradi ya kimkakati ya uchenjuaji ya (CIP)na (CIL) kwa mujibu wa Sheria ya Madini na kanuni zake.

#Vision2030: MadiniNiMaishaNaUtajiri
#InvestMineralValueAddition
#GDP:10% fromMineralSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals