[Latest Updates]: Stamigold Yaandika Historia Yaongeza Uhai wa Mgodi Hadi 2032

Tarehe : June 14, 2026, 8:46 a.m.
left

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yaipongeza kwa uwekezaji wa mitambo ya kisasa

Yatajwa kurefusha uhai wa mgodi kwa miaka sita zaidi kupitia ugunduzi wa mashapo mapya

Yatoa ajira 740 kwa wazawa, yagundua akiba mpya ya wakia 100,319

Bihalamuro

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Kampuni ya Uzalishaji Dhahabu ya STAMIGOLD inayosimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kufuatia mafanikio makubwa ya uzalishaji wa dhahabu na kurefusha uhai wa mgodi  hadi mwaka 2032.

Pongezi hizo zilitolewa  Juni 13, 2026 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, wakati wa ziara maalum ya wajumbe wa kamati hiyo iliyolenga kukagua shughuli za uzalishaji madini katika mgodi huo uliopo wilayani Biharamulo.

Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Mgalu aliitaka STAMICO kuendelea kufanya utafiti wa kina katika maeneo ya leseni zake zilizotengwa ili kupata taarifa mpya zitakazowezesha kuanzisha mgodi mwingine mpya wa dhahabu ili  kuendelea kuimarisha kampuni  ya STAMIGOLD.

Pia, alishauri STAMICO kuendeleza uwekezaji katika sekta ya madini kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan kwenye utafiti wa madini mkakati ili kuongeza idadi ya migodi itakayosaidia katika maendeleo ya uchumi kwa  taifa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, aliishukuru Kamati ya Bunge kwa ushauri wake wa kiufundi na kubainisha kuwa Wizara ya Madini itaendelea kupokea maoni na ushauri huo ili kuendeleza sekta, hususan kwenye maeneo ya ushirikiano wa kimkakati katika uwekezaji kupitia taasisi zake za utendaji.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Dkt. Venance Mwase, alieleza kuwa mgodi unaendelea na uhakiki pamoja na utafiti ndani ya leseni maalum ya uchimbaji kwa kutumia njia mbalimbali za ukusanyaji wa taarifa na ukadiriaji upya ili kuongeza taarifa za akiba ya mashapo ya mgodi huo.

Awali, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya kampuni hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa STAMIGOLD Ali Ali  alisema kuwa kuanzia mwezi Julai 2014 hadi Mei 2026, jumla ya wakia 137,049.73 za dhahabu zimezalishwa.

Ali  aliongeza kuwa, mgodi umefanikiwa kuongeza ufanisi kwa kununua mtambo mkubwa wa kisasa wa uchorongaji unaopunguza gharama za uendeshaji, pampu kubwa za kusukuma maji migodini, pamoja na kufanikiwa kutoa ajira za muda mfupi na mrefu kwa wazawa 740.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals