Tarehe : Aug. 22, 2023, 11:10 p.m.
Yatarajia kuimarisha uhusiano wa Kiuchumi na kidiplomasia
Kuibua fursa mpya za uwekezaji sekta ya madini
Ujumbe wa wafanyabiashara ya madini Tanzania ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo leo Agosti 23, umehitimisha ziara iliyoanza Agosti 12 hadi Agosti 23, 2023 katika miji mbalimbali ya kibiashara na uendelezaji madini nchini China.
Ziara hiyo ya wajumbe wapatao 100 kutoka sekta ya madini ukihusisha Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini (Femata), wafanyabiashara wa madini, watoa huduma migodini na wataalam kutoka taasisi za wizara ya madini likiwemo Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na taasisi za fedha.
Moja ya lengo la ziara hiyo ilikuwa kuongeza ushirikiano wa kisekta baina ya taifa la China na Tanzania hasa katika fursa za kiuchumi na kidiplomasia , biashara ya madini , kuongeza wigo wa soko la bidhaa zitokanazo na rasilimali madini na kubadilishana uzoefu wa kibiashara na matumizi ya tekinolojia.
Nchini China, ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali yanazojihusisha na biashara ya madini kama vile masoko ya madini, viwanda vinavyo chakata , kuchenjua , kuthaminisha madini na vinavyotengeneza mitambo na vifaa vya uchimbaji madini.
Aidha, ujumbe huo ulishiriki mazungumzo na makongamano ya kimkakati yaliyoshirikisha wadau wa Tanzania na China juu ya maendeleo ya sekta ya madini.
Kihistoria hiyo ni ziara ya kwanza nchini Tanzania iliyounganisha kwa pamoja wadau wa sekta ya madini , uongozi wa serikali , taasisi za fedha wenye lengo la kujadili na kufungamanisha fursa za kiuchumi kupitia mnyororo mzima wa sekta ya madini nchini.
Viongozi waliongoza ujumbe huo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Madini , Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Rais na Makamu wa Rais wa FEMATA
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.