Tarehe : March 23, 2022, 10:29 a.m.
ALIYOYASEMA WAZIRI WA MADINI DKT. DOTO BITEKO WAKATI AKIFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MKOANI MOROGORO TAREHE 23 MACHI, 2022*
*Tufanye kazi kwa uadilifu tuepuke vitendo vya rushwa*
# Napenda kuushukuru kwa dhati uongozi wa wizara kwa kunipa heshima ya kuzindua Baraza la Wafanyakazi ambalo ni la pili kuundwa baada ya Baraza la kwanza kumaliza muda wake wa miaka mitatu.
# Naahidi kushirikiana nanyi nyote watumishi wa wizara na taasisi zilizoko chini yake katika kuwezesha nchi yetu kunufaika na utajiri wa rasilimali madini ambazo Mungu ametujalia kuwa nazo kupitia mapato ya Serikali, ajira na fursa nyingine zinazoendana na utajiri huu.
# Sekta ya Madini ni moja ya Sekta ambayo tusipokuwa makini tutanyooshewa vidole. Tupambane na rushwa kwani inadhoofisha utoaji huduma, inaondoa haki kwa wananchi na kuleta manung’uniko tufanye kazi kwa uadilifu.
# Wizara haitamvumilia mtumishi yoyote atakayebainika na kuthibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa. Hakikisheni mnabeba dhamana hii na kutekeleza kikamilifu wajibu wenu kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kitaaluma na ya utumishi wa umma.
# Ushirikishwaji wa watumishi mahali pa kazi unaongeza morali ya kufanya kazi, kabla ya kuwalaumu jiulize unaowaongoza umewapa nini? wanajua mipango? miongozo? Sera? Ilani ya Uchaguzi? Baraza ndilo linaunganisha mawazo yaliyotawanyika ili yafanane. Mwenyekiti wa Baraza wasikilize wajumbe ili kuboresha mipango yetu bila watu kujiona duni.
# Msisahau kujadili namna ya kuimarisha ustawi wa wafanyakazi. Wakati wa kujitathmini ndani tujue kwamba wapo wengi wanatutathmini kutoka ndani na nje ya nchi.
# Nendeni mkawakumbushe watumishi mnaowaongoza hivi karibuni wizara inatimiza miaka 5 tangu kuanzishwa kwake, jifanyieni tathmini msibweteke na mafanikio yaliyopatikana, angalieni viashiria hatarishi mvifanyie kazi msirudi nyuma.
# Ninawapongeza wafanyakazi wa wizara kwa mafanikio tuliyoyapata , hadi sasa tumefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 406 kwa mwaka huu wa Fedha tunaoendelea kuutekeleza, kilichosababisha mafanikio haya ni mazingira mazuri ya biashara ya madini pamoja na kuwepo kwa Sheria nzuri ya madini.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.