[Latest Updates]: Wachimbaji Geita Wampongeza Rais Samia kwa Mafanikio Makubwa Sekta ya Madini

Tarehe : May 12, 2025, 7:57 p.m.
left

Wachimbaji Madini wapongeza upatikanaji wa Leseni na mazingira rafiki ya biashara

Waziri Mavunde aainisha mafanikio 16 ya Rais Samia kwenye sekta ya Madini

Aagiza uanzishwaji wa Soko la Dhahabu Katoro

RC Shigela aja na mikakati mizito ya kupaisha sekta ya madini Geita

Katoro,Geita

Wachimbaji na Wafanyabiashara wa Madini wa Mkoa wa Geita wamempongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia sekta ya madini katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Hayo yamesemwa jana kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wachimbaji hao katika eneo la mnada wa zamani Katoro,Geita kwa lengo la kumpongeza Rais Samia kwa mafanikio yaliyopatikana kupitia sekta ya madini.

Akitoa maelezo ya awali,Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini Mkoa wa Geita(GEREMA) Ndg. Titus Kabuo amesema dhumuni kubwa la kusanyiko hilo ni kumpongeza Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuiboresha sekta ya madini na kuweka mazingira rafiki ya uchimbaji na ufanyaji biashara hali inayopelekea kukua kwa shughuli za uchimbaji na kuathiri chanya maendeleo ya wachimbaji na uchumi wa nchi.

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimba Madini Tanzania(FEMATA) Ndg. John Bina amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia  sekta ya madini imeshuhudia mabadilko makubwa hasa katika upatikanaji wa Leseni kwa wachimbaji na hatua iliyoanzwa na serikali ya kufanya utafiti wa kina ili kuwaongoza vyema wachimbaji madini nchini.

Akiwasilisha hotuba yake,Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde ameyataja mafanikio 16 ya Rais Samia S. Hassan katika kuipaisha sekta ya madini kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kufikia 10.1%,ununuzi wa Dhahabu kupitia Benki Kuu,Kuongezeka kwa makusanyo ya maduhuli kuelekea lengo la kukusanya Shilingi Trilioni moja na upatikanaji wa mitambo ya kuchoronga 15 kwa ajili yaa wachimbaji wadogo.

Aidha, Waziri Mavunde ametumia fursa hiyo kukipandisha hadhi kituo cha ununuzi wa dhahabu cha Katoro na kuwa soko kamili la Dhahabu la Katoro.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wabunge Joseph Msukuma na Tumaini Magesa wamempongeza Rais Samia kwa kuweka mazingira rafiki ya biashara ambayo yamesaidia kupatikana kwa maendeleo makubwa na kukuza uchumi wa watu wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Martin R. Shigela amesema Mkoa wa Geita umejipanga kuchochea shughuli za madini kwa kuboresha mazingira ya uchimbaji ili kukuza uchumi wa  wananchi wa mkoa wa Geita kupitia upatikanaji wa Leseni zaidi ya 5308 na mitambo ya Uchorongaji ambayo Mh. Rais ameitoa kwa kwa wachimbaji wadogo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals