[Latest Updates]: Wanawake Wazidi Kung'ara Sekta ya Madini Tanzania

Tarehe : March 6, 2026, 10:55 a.m.
left

Kuelekea Machi 8, 2026

Wanawake Wazidi Kung'ara Sekta ya Madini Tanzania

Wafikia hatua kumiliki mgodi
Wanaonesha maono Sekta ya Madini.

Dodoma

Wakati dunia ikijiandas kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ifikapo Machi 8, 2026 , wanawake nchini Tanzania wameendelea kuandika historia mpya katika sekta ya madini wakivunja vikwazo vilivyodumu kwa miaka mingi.

Hayo, yamejihirisha kwa Asha Jama ambaye ni mmoja wa wamiliki wa mgodi wa MCC MAHADEO Tanzania unaochimba madini ujenzi aina ya kokoto katika kijiji cha Ntyuka jijini Dodoma.

Akizungumza na Madini Diary Asha Jama amesema kuwa, uwezeshaji wa wanawake katika sekta ya madini si tu suala la usawa wa jinsia , bali ni mkakati muhimu wa kukuza uchumi jumuishi.

Asha ameeleza kuwa, Wanawake wanaendelea kuwa sehemu ya uchumi na fursa za usawa zinaongeza juhudi katika uzalishaji sehemu mbalimbali pamoja na kuimarisha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.

Kwasasa wanawake tupo katika mnyororo mzima wa thaman madini tunajishughulisha katika kuleta na kuchangia Pata la Taifa kwa kufanya uzalishaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zilizopo katika mnyororo wote wa  thaman madini nchini.

Kwa upande Bi. Ellah Christopher ambaye anamiliki leseni ya madini ujenzi aina ya mchanga katika korongo la Ihumwa anasema kuwa , wanawake wana uwezo mkubwa katika kumiliki sekta ambazo zamani zilionekana kuwa za wanaume ikiwemo sekta ya madini na sekta za ujenzi hii ni kutokana na  mabadiliko ya kifikra na ushirikishwaji wa wanawake katika shuguli za maendeleo kumefungua mawazo chanya ambayo  yanaleta  maendeleo makubwa kuanzia ngazi ya familia, jamii inayotuzunguka na  taifa kwa ujumla.

Ellah anaeleza  kuwa, wanawake wengi ujifunza kupitia mifano ambapo mwanamke anayefanikiwa kwenye biashara kubwa anawatia moyo wanawake wengine lakini pia anaonyesha kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi na mfanyabiashara mkubwa.

Akifafanua kuhusu ushiriki wa mwanamke katika sekta za kiuchumi, amesema kuwa,  Mwanamke anayemiliki biashara kama mgodi wa mchanga ana jukumu kubwa la kuonyesha uwezo wa wanawake katika uchumi , kusaidia jamii pamoja na kulinda mazingira.

#WanawakeNaWasichana
HakiNaUsawa
#NiMsingiWaMaendeleo
#DiraYaTaifa2050

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals