[Latest Updates]: Serikali Kuendelea Kuweka Mazingira Rafiki Sekta ya Madini

Tarehe : Oct. 25, 2023, 5:27 p.m.
left

 Na.Wizara ya Madini- DSM

Serikali  imewahakikishia Wawekezaji Wakubwa , Wa kati na Wa dogo katika Shughuli za Madini  nchini kuwa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi katika mnyororo mzima wa Sekta  ya Madini kama Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inavyoelekeza.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 25, 2023 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Madini na Uwekezaji  Tanzania 2023 jijini Dar es salaam lenye kauli mbiu inayosema " Kuifungua Tanzania katika Fursa za Uwepo wa Madini"

Dkt.Biteko amesema kuwa  Serikali ipo kwenye mpango wa kufanya utafiti wa kina wa jiofizikia katika eneo lote la nchi ili kupata taarifa za aina ya miamba na madini yaliyopo ili kuwepo na Kanzidata ya taarifa itakayosaidia katika utafiti wa kina.

Dkt.Biteko amefafanua kuwa kuwepo kwa taarifa za utafiti kutawezesha kufungua migodi zaidi pamoja na kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi kwa kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi kama vile Maji na Kilimo.

Akielezea kuhusu uboreshaji wa miundombinu katika migodi mikubwa na midogo Dkt.Biteko ameeleza kuwa tayari mitambo mitano ya Uchorongaji miamba kwa wachimbaji wadogo imekabidhiwa na ifikapo mwezi juni 2024 mitambo mingine kumi itakabidhiwa.

Dkt.Biteko ameongeza kuwa mpaka sasa  zaidi ya  migodi 360 ya wachimbaji wadogo imeunganishwa na Nishati ya Umeme pamoja na kampuni kubwa 9  zimeingia ubia na Serikali katika utafiti na uchimbaji madini ya kimkakati yakiwemo madini ya Nikeli, Kinywe , Makaa ya Mawe.

Awali , Waziri wa Madini Mhe.Anthony Mavunde ameeleza kuwa Mkutano huu wa mwaka 2023 unatoa fursa kwa kampuni za madini kujadili kuhusu taarifa za namna ya  upatikanaji wa mitaji , Utafiti , Uchimbaji na Uchenjuaji na uwekezaji kwa kuzingatia mazingira rafiki baina ya Serikali na Taasisi na Kampuni binafsi.

Akizungumzia kuhusu umuhimu wa taarifa za jiolojia Mhe.Mavunde amesema uwepo wa taarifa za utafiti wa jiolojia na Jiofizikia  kutawezesha kujua aina ya mashapo yaliyopo na kuchimba kwa uhakika na kuwepo kwa uwekezaji wenye  uwiano sawa baina ya Serikali na Wadau wa Sekta ya Madini hasa katika  uvunaji madini kibiashara.

Kwa upande wake , Waziri wa Madini kutoka  nchi ya Mhe.Monica Chang'anamuno (MP), amesema kuwa  anaamini kupitia  jukwaa hili atajifunza mengi  juu ya mipango ya  maendeleo  ya sekta ya madini nchini Tanzania hasa kwenye madini ya Kimkakati na madini adimu.

Aidha , akielezea kuhusu mikakati ya Serikali ya Malawi kupitia Vision ya 2036 , ameeleza kuwa Serikali ya Malawi imefanikiwa kufanya utafiti wa Jiolojia kwa asilimia 80 na kugundua madini mbalimbali yakiwemo madini kimkakati na madini adimu ( Rare Earth Elements) ambayo yote yapo katika mpago wa uwekezaji.

Akielezea kuhusu utafiti wa kina  Waziri wa Madini wa Uganda Mhe . Lukeris amesema  jiolojia ya Afrika inatofautiana kidogo hivyo ni muhimu kufanya utafiti wa kina ili kubaini wingi na ubora wa madini yaliyopo katika sehemu husika kuwepo kwa taarifa za namna hiyo  kutarahisisha kuvutia wawekezaji bila kuhangaika na upembuzi yakinifu.

Akielezea mkakati wa sekta ya madini nchini Uganda Waziri Mhe. Peter Lukeris (MP) amesema  kwasasa Serikali ya Uganda kwa kushirikiana na sekta binafsi inaendelea na ukusanya wa taarifa za kina kwenye Madini na Mafuta ili kupata sahihi za uwekezaji.

Kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa utafiti wa Nishati ya Umeme kupitia madini ya Uraniam , Mhe.Waziri Lukeris  amezitaka Serikali za Afrika kuanza kufikiria kuzalisha Nishati umeme kupitia madini ya Uraniam kama Uganda ilivyoanza.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali akifungua Jukwaa ameeleza kuwa jukwaa hili ni sehemu ya Utekelezaji wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009 yenye lengo la kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini kwa kufanya majadiliano na kutoa mapendekezo ya namna gani ya kuboresha Sera ya Madini ya Mwaka 2009.

Akielezea maendeleo ya Sekta ya Madini , Mahimbali amefafanua kuwa Sekta imeendelea kukua ambapo kwasasa katika Pato la Taifa inachangia asilimia 9.1 kwa mwaka 2022.

Kwa upande wa kutoa ajira sekta ya Madini kwa mwaka 2021  ilitoa ajira 14308  na Mwaka 2022 kiwango kiliongezeka mpaka kufikia 16462.

Sambamba na hapo kuna ongezeka la mauzo ya bidhaa zitokanazo na madini mfanokwa mwaka 2021 mauzo yalikuwa bilioni 3.1 kwa mwaka 2022 yameongezeka kufikia mwaka 3.4.

VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals