[Latest Updates]: Tusimamie Vyema Rasilimali Madini kwa Ajili ya Maendeleo ya Nchi Yetu - Mavunde

Tarehe : Nov. 18, 2025, 1:59 p.m.
left

Ni utekelezaji wa maagizo ya Mh Rais Samia juu ya Utekelezaji wa miradi kupitia rasilimali za nchi

Asema Mradi wa Kuwaendeleza Wachimbaji Vijana, Wanawake Utatekelezwa*

Dkt. Kiruswa -   Matamanio ni kufikia Asilimia 15- 20 Mchango Pato la Taifa*

Katibu Mkuu Eng. Samamba Aahidi Ushirikiano*

Dodoma

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amewataka Watumishi wa Wizara ya Madini  na Taasisi zake kutambua kwamba maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Hassan kuhusu kutumia fedha za ndani zinazotokana  na rasilimali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo  ni agizo  linaloigusa  Wizara ya Madini moja kwa moja.

Ameyasema hayo Novemba 18, 2025 wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara ya madini na taasisi zake Makao Makuu ya Wizara Mtumba, mapema baada ya kuapishwa Ikulu ya Chamwino Dodoma na Rais  Dkt. Samia Hassan.

‘’Mapato ya ndani aliyoyaelekeza Mhe.  Rais yanatugusa sisi Sekta ya Madini moja kwa moja. Dkt. Samia anataka uongozi unaogusa watu hivyo tuendelee kuongeza kasi. Lakini Katibu Mkuu nitapenda maelekezo aliyoyasema wakati akihutubia Bunge, haya ya leo na yale yaliyoahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi yamfikie kila mtumishi,’’ amesisitiza Mavunde.

Mhe. Mavunde ameeleza kuwa Rais. Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa na imani kubwa na Wizara ya Madini hususan kutokana na mapato yanayotokana na  rasilimali madini kuendesha uchumi wa nchi  na hivyo kumtaka kila mtumishi kutumia nafasi yake kuhakikisha sekta ya madini inagusa maisha ya kila mwananchi kwa manufaa ya jamii na taifa.

Akielezea kuhusu programu ya Mining for A Brighter Tommorrow (MBT), Mhe. Mavunde amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kikamilifu kama ulivyopangwa kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji vijana na wanawake kuchimba kwa tija. Kupitia mradi wa MBT Wizara imepanga kuwawezesha vijana na wanawake kwa kuwapatia maeneo ya kuchimba na teknolojia ili kuwarahisishia shughuli zao.

Pia, ametumia fursa hiyo kumshukuru Dkt. Samia kwa kumuamini na kumrejesha tena kuitumika wizara hiyo pamoja na kuwashukuru watumishi wote na wadau wote wa Sekta ya madini  kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika kipindi cha miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo na kueleza kwamba, kwake mlango uko wazi kwa  ajili ya kupokea maoni na mapendekezo yanayojenga kwa lengo la kuendelea kuboresha Sekta ya Madini.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa Dkt. Kiruswa ameshukuru Rais Samia kwa kumuamini kuendelea kuhudumu katika Wizara ya Madini na kuwashukuru watendaji wote kwa ushirikiano waliompatia na kuwapongeza watumishi kwa kazi wanayofanya hususan kuendelea na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.

‘’Mhe. Rais ametoa mwelekeo, hivyo tunapaswa  kutekeleza yale  tuliyoagizwa,  tuliwaacha na mchango wa asilimia 10.1 matamanio ni kufikia  asilimia 15 – 20  ifikapo mwaka 2030’’ amesema Dkt. Kiruswa.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Madini Eng. Yahya Samamba amewapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa tena katika Wizara ya Madini na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano wa utendaji kazi  kuanzia ngazi ya chini mpaka juu.

Pamoja na mambo , Kamishna wa Madini Dkt.AbdulRahman Mwanga kwa pamoja  amewapongeza  hao  kwa kuchaguliwa tena na kuahidi  ushirikiano

*#Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri*

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals