[Latest Updates]: Madini 2030 Kutangazwa na Timu ya Madini Iringa

Tarehe : Sept. 26, 2023, 8:01 a.m.
left

#Waahidi kufanya vizuri na kurejea na mataji

Watumishi wa Wizara ya Madini wanaoshiriki mashindano ya Shirikisho la  Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) wametakiwa kubeba na kuutangaza Mwelekeo Mpya wa Wizara  Maono 2030; Madini ni Maisha na Utajiri kipindi chote watakachokuwa wakishiriki michezo hiyo mkoani Iringa. 

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Madini, Augustine Olal kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Madini wakati akiwaaga Watumishi wa Wizara wanaotarajiwa kushiriki mashindano ya SHIMIWI kuanzia Septemba 27, 2023 hadi Oktoba 14, 2023.

Amesema kuwa hiyo ndio fursa ya kipekee kutangaza mwelekeo huo mpya kupitia michezo.

“Wote tunafahamu kuhusu Mwelekeo Mpya wa Wizara yetu, Maono 2030; Madini ni Maisha na Utajiri, tunaomba mkatangaze vizuri Mwelekeo wetu huu huko mlipo kwa muda wote, mtusaidie kututangazia, hiyo ndiyo kaulimbiu yenu muda wote mkisalimiana hata mkishangilia ushindi mtakaokuwa mnaupata, tunataka kila mmoja ajue kuhusu kaulimbiu yetu hiyo" amesema Olal. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Rasilimaliwatu, Beatrice  Matemu amewataka Watumishi hao kwenda kushiriki mashindano hayo kwa lengo la kuibuka washindi sambamba na kutangaza kazi nzuri ya wizara.

Naye, Kiongozi wa msafara wa Wanamichezo hao John Issangu ameahidi kwenda kutangaza mwelekeo huo mpya wa Wizara na kwamba watakituma kwa bidii ili warejee na makombe katika michezo watakayoshiriki.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals