[Latest Updates]: Nemc, Osha na Halmashauri Zatakiwa Kuwasimamia Wachimbaji Wadogo

Tarehe : June 15, 2025, 5:41 p.m.
left

Ruangwa, Lindi

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC), Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) na Halmashauri za Mji zatakiwa kuwasimamia na kuwaelekeza wachimbaji wadogo wa madini namna  bora ya kuchimba madini bila kuharibu mifumo yoyote ya mazingira pamoja na kuzingatia Usalama wa Afya mahali Pa kazi wakati wa shughuli za uchimbaji madini zinafanyika.

Hayo yamesemwa Juni 14, 2025 na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa  wakati anafunga maonesho ya madini na fursa za uwekezaji wilayani Ruagwa kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Dkt. Kiruswa alisema kuwa, Serikali inazipongeza taasisi zote zilitoa mafunzo mbalimbali wakati wa maonesho kwa wachimbaji wadogo wa madini yaliyohusu namna ya  bora uchimbaji na uchenjuaji madini kwa kufuata mifumo ya kitaalamu pamoja maendeleo  ya Sayansi na teknolojia.

Dkt.Kiruswa aliongeza kuwa,  Serikali itaendelea kutoa leseni kwa wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali  yaliyofanyiwa utafiti wa jiosayansi ili kuwasaidia wachimbaji wadogo kufanya uchimbaji katika maeneo yenye tija bila kupoteza mitaji kama Vision 2030 inavyosema, Madini ni Maisha na Utajiri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alisema kuwa, Mkoa wa Lindi utaendelea kutangaza fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini ili kuongeza uwekezaji unaofungamanisha  Sekta ya Madini na Sekta  nyingine za kiuchumi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Lindi  na mikoa jirani inayopakana na Lindi.

Naye, Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Lindi Mayunga Mussa aliipongeza Wizara ya Madini kwa kazi nzuri inayofanya hususan katika kusimamia na kuendeleza Sekta ya Madini ambapo katika  kipindi cha mwaka 2019 hadi 2020 makusanyo ya maduhuli kwenye Sekta ya Madini yalikuwa shilingi bilioni 1.5 mkoani Lindi ila sasa yameongezeka mpaka kufikia shilingi bilioni 8.1 kwa mwaka 2024/2025.

Maonesho hayo yalifanyika kwa  Kaulimbiu inayosema "Madini na Uwekezaji Fursa za Kiuchumi Lindi , Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025"

#Vision2030:MadiniNiMaishaNaUtajiri
#DGP: 10.1%From MineralSector
#InvestInMineraSectorTz

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals