Tarehe : Nov. 25, 2025, 1:27 p.m.
Ni Leseni za Utafiti na Uchimbaji Madini wa Kati.
Ni maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuwezesha Vijana
Waziri Mavunde aelekeza zielekezwe kwenye Programu ya MBT na wawekezaji walio tayari
Eneo la ekari 741,494 lilihodhiwa bila kufanyiwa kazi
DODOMA
WAZIRI wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde ameilekeza Tume ya Madini kufuta leseni 73 za uchimbaji wa kati na utafiti wa madini ambazo hazijaendelezwa.
Mhe. Mavunde ametoa maelekezo hayo leo Novemba 25, 2025 wakati akiongea na vyombo ya habari katika ukumbi wa Ofisi za Tume ya Madini mjini Dodoma.
Mhe. Mavunde amesema kuwa , ufutaji wa leseni hizo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuiwezesha Wizara ya Madini kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa na kuhakikisha rasilimali madini zinawanufaishaWatanzania na Taifa kwa ujumla.
Mhe. Mavunde ameongeza kuwa, eneo lenye ukubwa wa ekari 741,494 lilihodhiwa bila kufanyiwa uendelezaji wowote , jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madini , Sura 123.
Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Leseni zilizofutwa ni pamoja na leseni za utafutaji wa madini 44 na leseni 29 za uchimbaji wa Kati kutokana na kushindwa kurekebisha makosa yao.
Akielezea kuhusu matumizi ya maeneo yote yaliyofutwa, Mhe. Mavunde amesema kuwa, maeneo hayo yatapangwa kwa ajili ya mradi wa vijana katika programu ya Mining Better Tomorrow (MBT) ili waweze kunufaika na rasilimali madini.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.