[Latest Updates]: Rais Samia Ameipongeza Wizara ya Madini kwa Kuisimamia Sekta

Tarehe : Oct. 20, 2022, 10:15 a.m.
left

Atoa maagizo kwa Wizara ya Madini*

Asema Mkoa wa Geita ni kinara wa dhahabu*

Asisitiza viwanda vya kusafisha dhahabu kisasa vipo hapa Tanzania*

Serikali kuangalia upya tozo zinazotozwa katika viwanda vya kusafisha madini*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Madini kwa kuendelea kufanya vizuri katika kuisimamia Sekta hiyo hapa nchini ili iwe chachu ya kitovu cha uchumi.

Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Geita katika uwanja wa shule ya msingi Kalangalala Rais Samia amesema Wizara ya Madini inafanya vizuri katika usimamizi wa Sekta hiyo lakini inapaswa kuongeza bidii hususan katika kutoa elimu ya Sheria na Kanuni za madini kwa wachimbaji.

Aidha, amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wananchi wa mkoa wa Geita katika ujenzi wa uchumi hususan kwa kupitia shughuli za uchimbaji wa madini.

"Ni kweli kabisa kiwango kikubwa cha madini ya dhahabu kinapatikana hapa Geita na inachimbwa ndani ya mkoa wa Geita, mchango wa mkoa wa Geita ni zaidi ya asilimia 50 ya dhahabu yote inayochimbwa Tanzania," amesema Rais Samia.

Mara baada ya kuzindua kiwanda cha kusafisha dhahabu, Rais Samia amewataka wanachi wa Geita na mikoa yote inayochimba madini ya dhahabu kuvitumia viwanda vya kisasa vya kusafisha na kuchenjua dhahabu vilivyopo nchini mara baada ya kuzindua kiwanda cha Mama Masasi cha Geita.

"Niombe sana tupeleke dhahabu zetu huko zikachenjuliwe ili Tanzania iongeze thamani ya madini ya dhahabu yenye thamani kubwa," amesisitiza.

Vile vile, ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha shughuli za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji na biashara za madini zinafanywa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo inayosimamia Sekta ya Madini.

Vile vile, Rais ameitaka wizara kuendelea kutoa elimu juu ya Sheria ya Madini na Kanuni zake kwa wadau mbalimbali kupitia mafunzo maalum.

Rais Samia ameitaka Wizara ya Madini kuendelea kushirikiana na idara nyingine za Serikali na vyombo vya Dola mkoani na katika sehemu nyingine ambayo kuna uchimbaji mkubwa katika kusimamia shughuli za uzalishaji na biashara ya madini na kudhibiti vitendo vya utoroshaji wa madini.

Pia, ameagiza wizara kuendelea kuwaunganisha wachimbaji wadogo na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa lengo la kupata taarifa za kijiolojia yenye madini, elimu ya masuala ya utafiti, uchimbaji na uchenjuaji ili kuongeza tija kwenye shughuli zao.

Kuhusu suala la kodi kwa wachimbaji ameiagiza Wizara ya Madini kukutana na Wizara ya Fedha kuziangalia na kuwasikiliza wadau na wafanyabiashara kuhusu kodi zinazoleta kero na kupunguza kasi ya utendaji kwa wawekezaji wanaowekeza katika Sekta hiyo.

Naye, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema, mkoa wa Geita ni mkoa kinara wa dhahabu nchini. Ameongeza Geita ni ya kwanza katika mikoa inayozalisha dhahabu hapa Tanzania.

Dkt. Biteko amemhakikishia Rais Samia kuwa Sekta ya Madini itafikia lengo la makusanyo iliyopangiwa kupitia miradi mbalimbali ya uchimbaji madini inayoendela sasa katika maeneo mbalimbali.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals