[Latest Updates]: Tanzania Ina Mengi ya Kujifunza Afrika Kusini - Balozi Bwana

Tarehe : Feb. 4, 2024, 8:32 a.m.
left

CapeTown

Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. James Bwana amesema Tanzania inayo mengi ya kujifunza kwenye Mkutano wa Uwekezaji wa Madini Barani Afrika wa Mining Indaba utakaofanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Februari, 2024 nchini Afrika Kusini.

Mbali ya kuwa Balozi wa Afrika Kusini pia, Mhe. balozi Bwana anaiwakilisha Tanzania katika nchi za Jamhuri ya Botswana na Ufalme wa Lesotho.

Ameyabainisha hayo leo Februari 4, 2024 wakati akizungumza katika mahojiano maalum baada ya kuzungumza na Ujumbe wa Tanzania unaotarajia kushiriki katika Mkutano huo utakaofanyika katika Hotel ya Westin ambapo mwaka huu unatimiza miaka 30 tangu kuanza kwake.

Amesema Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa madini Afrika na duniani inatarajia kunufaika vilivyo kupitia mkutano huo na hususan kujifunza mengi kutoka katika nchi ya Afrika Kusini ambayo imepiga hatua kubwa katika masuala mbalimbali kwenye mnyororo wa shughuli za madini ikiwemo yanayohusu uwekezaji kwenye sekta ya madini, teknolojia shughuli za uongezaji thamani madini pamoja na namna nchi hiyo inavyosimamia sekta ya madini.

Aidha, ameongeza kwamba, mbali na kujifunza kutoka katika nchi ya Afrika Kusini na mataifa  mengine, pia Tanzania inatarajia kuutumia mkutano huo kunadi fursa zake za uwekezaji  zilizopo katika Sekta ya Madini.

'' Wenzetu katika Jamhuri ya Afrika Kusini wamepiga hatua kubwa katika sekta ya madini kwa hiyo kama nchi tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao na kutoka kwa nchi nyingine zinazoshiriki mkutano huo. Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi duniani ambazo zinafanya vizuri katika Sekta ya Madini na Rasilimali Madini imechangia kuwafikisha hapa," amesema balozi Bwana.

 Wakati mkutano huo unatarajia kufunguliwa rasmi kesho Februari 5, 2024, leo Mawaziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaosimamia masuala yanayohusu madini wanakutana katika Kongamano kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Sekta ya Madini Barani Afrika.

Kwa upande wa Tanzania, Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa anaongoza ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo, akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe. Bwana, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Msafiri Mbibo, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Dkt. Mussa Budeba.

Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano wa Uwekezaji wa Mining Indaba kwa  kushirikiana na Sekta binafsi inayowakilishwa na Chemba ya Migodi Tanzania ambapo kampuni mbalimbali zilizo chini ya mwanvuli huo zinashiriki.


#TANZANIA@The Mining Indaba    #InvestinTanzaniaMiningSector

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals