[Latest Updates]: GST Yaja na Teknolojia ya Kisasa ya Utafiti wa Madini kwa Bei Nafuu

Tarehe : Sept. 24, 2025, 11:07 a.m.
left

Wachimbaji Wadogo Waaswa Kuchangamkia Fursa za Utafiti katika Leseni Zao kwa Gharama Nafuu.

 Geita

Kwa muda mrefu Wachimbaji Wadogo wamekuwa wakichimba kwa kubahatisha, mara nyingine wakipoteza mitaji yao yote kwa sababu ya kukosa taarifa za uhakika kuhusu maeneo yenye rasilimali. Lakini Serikali sikivu imeleta suluhisho la kudumu.

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeendelea kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Madini kupitia huduma za utafiti wa madini kwa teknolojia ya kisasa, zikiwa na gharama nafuu inayowalenga hasa kundi la Wachimbaji Wadogo. Lengo likiwa kuondoa uchimbaji wa kubahatisha na kuhakikisha kila shilingi inayowekezwa inaleta matokeo.

Akizungumza mapema leo Septemba 24, 2025, Mfizikia Mkuu wa GST, Octavian Minja amewasisitizia wachimbaji wadogo wanaotembelea banda la GST katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili – Geita, kuwa ni muhimu kufanya tafiti za jiosayansi kabla ya kuanza uchimbaji ili kuongeza uzalishaji na kuepuka hasara. 

“Wachimbaji wadogo wanapaswa kuchangamkia fursa hii. Kupitia huduma zetu, wanaweza kupata taarifa za kitaalamu kabla ya kuwekeza mitaji yao. Hii itapunguza hasara na kuongeza tija,” anasisitiza Minja.

Anabainisha kuwa wachimbaji wengi wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na taarifa sahihi za jiosayansi zinazoonesha miamba, madini na mwelekeo wa miamba husika, hali inayowasababisha kuchimba kwa kubahatisha na kupoteza mitaji.

Kwa mujibu wa Minja, GST inatumia vifaa vya kisasa vya jiofizikia vinavyoweza kubainisha aina ya miamba iliyopo chini ya ardhi na mwelekeo wa miamba iliyobeba madini. “Tunawaalika wachimbaji wote nchini kuitumia GST hususan katika hatua ya utafutaji ili kuepuka kupoteza mitaji na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchimbaji holela,” anasisitiza Minja.

Huduma hizi zimeletwa mahsusi kuendana na uwezo wa kifedha wa wachimbaji wadogo, huku zikitoa matokeo sahihi na ya haraka. Tayari wachimbaji waliotembelea banda la GST wameonesha shauku kubwa, wakieleza kuwa hii ndiyo fursa waliyoisubiri kwa muda mrefu.

Kwa maneno mengine, GST imekuwa daraja kati ya teknolojia ya utafiti  na mchimbaji mdogo. Matokeo yake ni uchimbaji wa uhakika, mitaji salama, na uchimbaji wenye tija.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals