[Latest Updates]: Sheria ya Madini Sura Namba 123 Kufanyiwa Marekebisho

Tarehe : Aug. 2, 2023, 2:11 p.m.
left

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amefungua Kikao kazi kupokea maoni ya wadau wa Sekta ya Madini kuhusu mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria ya Madini Sura Namba 123 pamoja na baadhi ya Kanuni zake.

Dkt. Biteko amefungua kikao hicho kitakachoendeshwa kwa siku tatu katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam kilichohudhuliwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini nchini.

"Tuliona tusijifungie wenyewe ofisini kutengeneza Sheria tukaamua kuwaita wadau wa sekta hii ili mtoe mapendekezo yenu yatakayosaidia  kurekebisha Sheria ya Madini Sura namba 123 na Kanuni zake ili kuboresha utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Madini," amesema Dkt. Biteko.

Pamoja na Mambo mengine, Dkt. Biteko ameyataja maeneo ambayo tanayohitaji kuboreshwa ni pamoja na Kanuni ya Masoko ya Madini, Kanuni ya Eneo Tengefu la Mirerani, Kanuni ya Uchenjuaji Madini, Kanuni ya Haki Madini, Kanuni ya Uongezaji Thamani Madini na mapendekezo ya Kanuni mpya ya Uchenjuaji Mdogo wa Madini ili kuboresha shughuli za Sekta ya Madini na kurejesha Minada ya Madini ya Vito.

Aidha, Dkt. Biteko amewataka watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake kupokea maoni ya kila mdau ili kuhakikisha maboresho ya Sheria na Kanuni zilizo kusudiwa yanakuwa na manufaa kwa Serikali na kwa watanzania.

Naye, Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga amesema ili kuweza kuikuza Sekta ya Madini lazima tuzingatia Sheria na Kanuni ili ziweze kuisimamia Sekta na kama kuna mapungufu ni vyema ikarekebishwa mapema.

“Nakumbuka Mheshimiwa Waziri alitueleza kwamba hatokuwa tayari kupeleka Bungeni mapendekezo ya madiliko ya Sheria na Kanuni zake kama hatuta washirikisha wadau wa madini na sisi tulifuata maelekezo yako na leo tumewaita wadau wetu ili wachangia maoni katika kuboresha Sheria yetu ya Madini na baadhi ya Kanuni,” amesema Dkt. Mwanga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chemba ya Migodi, Mhandisi Filbert Rweyemamu amempongeza Dkt. Biteko kwa kuwashirikisha wadau wa Sekta ya Madini katika kutoa maoni yao ili kuboresha Sheria na Kanuni za sekta hiyo.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals