[Latest Updates]: Aliyoyasema Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihitimisha Bunge la 12 jijini Dodoma Juni 27, 2025

Tarehe : June 27, 2025, 2:24 p.m.
left

Aliyoyasema Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihitimisha Bunge la 12 jijini Dodoma Juni 27, 2025
Sekta ya Madini

#Kutokana na Maboresho ya Sheria ya Madini Sura ya 123, imewezesha Benki Kuu ya Tanzania ( BoT) kununua kilo 3,424 za dhahabu zenye thamani ya shilingi bilioni 702.3.

#Tumeongeza masoko ya Madini na Vituo vya ununuzi wa Madini kutoka 61 Mwaka 2022 kufikia 109 na Masoko ya Madini kutoka 41 kufikia 43.

#Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi imeanzisha Viwanda vya Kusafisha Dhahabu 8 kwa viwango vya Kimataifa ambavyo vipo mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam, Geita na Chunya.

#Tunaendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa ( STAMICO) kama nilivyoahidi ili liwekeze kwa niaba ya Serikali.

#Habari njema ni kwamba, Sekta ya Madini ilifikia asilimia 10 mwaka 2024 kutoka asilimia 6.8 mwaka 2020.

#Serikali imeboresha hali za wachimbaji wadogo kwa kutekeleza ahadi ya kuwaendeleza kwa kuwanunulia mitambo ya uchorongaji ambayo tumeisambaza maeneo mbalimbali. Kwa sasa wachimbaji Wadogo  wanaochangia asilimia 40 ya mapato yote ya madini.

#Aidha, Serikali imefuta leseni za maombi 2648 ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata maeneo halali ya uchimbaji ili wazidi kuimarika.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals