Tarehe : July 6, 2025, 12:32 p.m.
Dar es Salaam, Julai 6, 2025
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Cyprian Luhemeja, ameipongeza Tume ya Madini kwa hatua yake ya kutoa leseni za uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo huku ikizingatia vigezo vya utunzaji wa mazingira.
Ameitaka Tume kusimamia kikamilifu utekelezaji wa masharti ya leseni ili kuhakikisha mazingira yanalindwa ipasavyo.
Akizungumza wakati wa ziara yake katika Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam, Mhandisi Luhemeja amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuondoa uchimbaji holela na kupunguza uharibifu wa mazingira.
“Zamani wachimbaji wadogo wa madini walikuwa wanaingia kwa nguvu kwenye maeneo ya uchimbaji bila kufuata utaratibu wowote, na mara nyingi kuchimba bila kuwa na leseni. Hali hii ilisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira,” amesema Mhandisi Luhemeja.
Kwa upande wake, Afisa Sheria Mwandamizi wa Tume ya Madini, Bw. Damian Kaseko, amesema Tume inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Madini, ikiwa ni pamoja na kutoa leseni za uchimbaji, kusimamia biashara ya madini nchini, pamoja na kusuluhisha migogoro ya ardhi katika maeneo ya uchimbaji wa madini.
Bw. Kaseko ameeleza kuwa utoaji wa leseni za madini kwa wachimbaji wadogo unazingatia taratibu madhubuti, ikiwemo kuwasilisha Mpango wa Utunzaji na Uendelezaji wa Mazingira (Environmental Protection Plan - EPP) kabla ya kuidhinishiwa leseni ya uchimbaji katika eneo husika.
by: madini
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…
by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…
by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.
’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…
by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…
by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.