[Latest Updates]: Waziri Mavunde Atembelea Mradi wa Lindi Jumbo

Tarehe : Dec. 28, 2023, 10:16 a.m.
left

 Ujenzi wake wafikia zaidi ya asilimia 90 

 Kuanza uzalishaji mapema Machi, 2024 

 LINDI 

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde leo Desemba 28, 2023 ametembelea mradi wa Lindi Jumbo Limited uliopo Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa mgodi wa madini ya kinywe (graphite)

Awali akielezea maendeleo ya ujenzi wa mgodi huo, Meneja wa Mradi, Chediel Mshana ameeleza kuwa mradi huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa uchenjuaji umefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo uzalishaji wa   madini ya kinywe unatarajia kuanza mapema Machi, 2024.

Ziara hii ni sehemu ya ziara za Waziri Mavunde zenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini nchini sambamba na kutatua changamoto mbalimbali.

Katika ziara yake ameambatana na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi kutoka Tume ya Madini na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Dickson Joram

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals