[Latest Updates]: Kijiji cha STAMICO Sabasaba Chavuta Wengi

Tarehe : July 4, 2025, 12:16 p.m.
left

Kijiji cha  Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na wadau wake kimekuwa kivutio kikubwa kwa wageni wengi wanaotembelea Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) yaliyoanza tarehe 28 Juni,2025.

Shirika limeendelea kuinadi nishati safi na salama ya kupikia ya Rafiki Briquettes pamoja na shughuli za uchimbaji madini.

 STAMICO inashiriki katika maonesho haya kwa lengo la kutangaza miradi na bidhaa za STAMICO ili wageni wanaotembelea banda la Shirika waweze kununua na kushiriki katika mnyororo wa usambazaji wa bidhaa za STAMICO.

Washiriki waliopata bahati ya kutembelea banda la STAMICO akiwemo  Bi. Lulu Mwilima, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Walemavu Tanzania  alionesha kuvutiwa na shughuli zinazofanywa na Shirika hasa kwa kuwahusisha Watanzania katika usambazaji wa nishati ya  Rafiki Briquettes.

Ameomba STAMICO ishirikiane na taasisi yake yake kusambaza  bidhaa za Shirika na hasa nishati ya Rafiki Briquettes.

Jumanne Hamis,mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam amesema nishati ya Rafiki Briquettes imemvutia sana na kuomba Shirika liongeze juhudi kuitangaza.

Wageni wengine waliotembelea Kijiji cha STAMICO pia wamevutiwa na huduma mbalimbali kwa wadau washiriki 

Wadau wanaoshiriki na STAMICO eneo moja ni pamoja na Wizara ya Madini,Tume ya Madini,Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake (TAWOMA) na Shirikisho la Wachimbaji Wadogo (FEMATA).

Wadau wengine ni pamoja na Kikundi cha Wanawake na Samia na Kituo cha Gemolojia na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika  Rasilimali za Madini,Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).

STAMICO inashiriki maonesho haya ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wake mpya wa mwaka wa fedha 2025/2026 unaoitwa MASTASHA (Make STAMICO Shine Again).

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals