[Latest News]: Mawaziri Afrika Wajadili Madini Mkakati

Tarehe : Oct. 7, 2022, 11:20 a.m.
left

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameshiriki Mkutano wa Pili wa Mawaziri wa Madini Afrika uliondaliwa na Umoja wa Afrika na kufanyika Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mkutano huo umelenga kujadili mkakati wa pamoja wa nchi za Afrika kuhusu ugunduzi, uendelezaji na uvunaji madini mkakati hasusan green energy minerals  ambayo yanahusisha madini ya Lithium, Nickel, Copper, Graphite, Manganese, cobalt, Vanadium ambayo ni muhimu kwa nishati ya magari ya umeme, umeme wa solar, batteries aina zote, transformer za umeme kwa lengo la kupunguza kiwango cha carbon kwenye anga.

Maadini mengine ya kimkakati  yaliyojadiliwa katika mkutano huo  ni madini teknolojia ambayo ni  REE, PGE, Phosphate, Niobium Tin. 

Aidha, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuangalia Sera, Sheria na  Kanuni zinazowezesha kuongeza manufaa kwa nchi za Afrika na wananchi wake kutilia mkazo suala la uongezaji thamani madini mkakati hadi zao la mwisho.

Vilevile, Serikali za nchi za Afrika zimehimizwa kujikita katika utafutaji madini badala ya kuziachia sekta binafsi haususan kampuni za kigeni pekee.

Mfano umetolewa kwa nchi ya Namibia ambayo Serikali yake kupitia Taasisi yake ya Jiolojia  imefanikiwa kufanya utafiti wa  madini nchi nzima  ambapo  hadi sasa Pato Kuu la Taifa hilo linategemea uchumi wa madini.

Mbali na hayo, mkutano huo umebainisha changamoto zinazozikabili nchi nchi za Afrika katika sekta hiyo  kuwa ni kutokana na kuwepo kwa  changamoto zinazotokana na  uwezo mdogo wa mitaji, uwezo mdogo wa kufanya tafiti za madini na teknolojia ndogo ya kuongeza thamani madini.

Mkutano huo umehudhuriwa  na Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi za Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Senegal, Sudani Kusini, Ethiopia, wawakilishi kutoka nchi za Namibia na Botswana pamoja na  wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira na utafutaji madini.

Katika mkutano huo, Dkt. Kiruswa aliongozana na Meneja wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Maswi M. Solomon

 

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals