[Latest Updates]: Waziri Mavunde Akutana na Wadau wa Kimataifa Indaba Kuvutia Uwekezaji

Tarehe : Feb. 10, 2026, 9:17 p.m.
left

Capetown- Afrika Kusini

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde anayeongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kongamano la Mining Indaba akiongozana na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Msafiri Mbibo na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Mhe. James Bwana wamefanya vikao vya pembeni Februari 9, 2026 na viongozi, wawekezaji na kampuni kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kuboresha mahusiano, kuvutia uwekezaji na kukuza sekta ya madini nchini Tanzania.

1. MKUTANO NA WAZIRI WA MASUALA YA BIASHARA NA UCHUMI WA FINLAND MHE. SAKARO PUISTO 

Mkutano huu umelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Taasisi ya Jiolojia ya Finland (GTK) na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kupitia MoU ili:-
 Kuwajengea uwezo watalaamu katika kuchambua, kutafsiri na kuhakiki ubora wa taarifa za Jiosayansi nchini Tanzania.

  Kujenga uwezo wa watalaamu wa GST katika kuendesha maabara hususan upimaji wa sampuli kwa viwango vya kimataifa.

  Kushirikiana kwenye Utafiti wa jiosayansi hususan High Resolution Geophysical Surveys.

2.  KIKAO NA TAASISI MBALIMBALI KUTOKA SERIKALI YA MAREKANI

Ujumbe wa Taasisi kutoka Nchini Marekani uliongozwa na Naibu Mkurugenzi na Mkuu wa Shughuli za Uendeshaji za Shirika la Maendeleo ya Biashara la Watu wa Marekani (USTDA), Bw. Thomas Hardy. Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya Marekani  na Tanzania ikiwemo:-
   Utafiti na uongezaji thamani wa madini muhimu na madini mkakati nchini Tanzania.

   Umuhimu wa tafiti za kina za jiosayansi zinazohusisha kurusha ndege. 

   Maendeleo ya mradi wa utafiti wa madini ya kinywe kwa kushirikiana na GST katika leseni zinazomilikiwa na STAMICO.

  Umuhimu wa uongezaji thamani madini ndani ya nchi kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura 123 

Mhe. Waziri ameeleza umuhimu wa kufanya tafiti za kina na kusisitiza kuwa ni vyema Serikali ya Marekani ikaweka mkazo katika eneo hili ili kuwezesha uanzishwaji wa miradi mingi kwenye sekta ya madini nchini. Aidha, Mhe. Mavunde amebainisha kuwa, utaratibu wa kufanya tafiti za kina kwa kushirikiana na GST ukawa endelevu ili kupata taarifa zaidi za kina za kuwezesha kuanzisha miradi mikubwa ya uchimbaji madini.

3. MKUTANO NA TAASISI YA RIO TINTO YENYE UZOEFU WA ZAIDI YA MIAKA 150 KATIKA SEKTA

Uwepo wa miundombinu ya Reli ya Kisasa (SGR) Shirika la Pamoja la Serikali ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Sera ya Madini, mazingira wezeshi ya kibiashara Sekta ya Madini Tanzania yametajwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyoivuta Kampuni ya Kimataifa ya Rio Tinto yenye uzoefu wa miaka 150 kwenye shughuli za madini kuonesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Madini nchini. Kampuni hiyo inafanya shughuli zake katika nchi takribani 35 duniani na imejikita katika utafiti na mnyororo wa thamani wa madini ya Shaba, Bauxite Aluminium na Graphite.  Mhe.Mavunde amesisitiza kuwa;

Rio Tinto imeshauriwa kuwezesha kufanyika utafiti kwa haraka na ifanye mazungumzo na STAMICO ambao wanamiliki leseni za utafiti kwenye madini wenye uhitaji nayo ili wafanye kwa pamoja na kuwezesha kuanza shughuli za uchimbaji kwa wakati.

Kwa mujibu wa Sheria, STAMICO wanaruhusiwa kuingia ubia na wawekezaji ndani na nje ya nchi, hivyo Rio Tinto wana nafasi kubwa na wanakaribishwa nchini Tanzania ili kuwekeza kwenye utafiti na baadaye kuanzisha mgodi wa kimkakati ambao utahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuongeza thamani ya madini hayo nchini.

by: madini

Latest News
Biteko atoa wito Mabenki ya ndani kuungana kukope…

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyataka Mabenki ya ndani kushirikiana ili kuweza kuzikopesha kampun…

by: madini on: April 23, 2021, 5:11 a.m.

Ukusanyaji wa Maduhuli Sekta ya Madini Wafikia As…

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai, 202…

by: madini on: April 28, 2021, 12:51 p.m.

Aliyoyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Adol…

’Nimeona Nyuso Zenye Furaha , Amani na Utulivu’’ Ninayo furaha kuwa nanyi hapa ili tuanze safari hi…

by: madini on: Jan. 10, 2022, 2:55 p.m.

Tume ya Madini Yaagizwa Kutafuta Masoko

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Tume ya Madini kutafuta Masoko ya wanunuzi wa…

by: madini on: Jan. 30, 2022, 9:32 a.m.

Read News
Contact Us
Permanent Secretary,
Ministry of Minerals,
Madini Street,
Government City, Mtumba
P. O. Box 422,
Dodoma, Tanzania
Email: ps@madini.go.tz
Copyright©2021 Ministry of Minerals