Mazingira
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 7 Oktoba, 2017 alibadilisha Tangazo la Ugawaji wa Majukumu ya Wizara (Kiambatanisho) Na.144 la 22 Aprili, 2016. Katika marekebisho hayo, Rais ameunda Wizara ya Madini yenye wajibu wa kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Sera za Madini; Migodi, Uchunguzi wa Jiofizia na Jiolojia; Masuala ya Tume ya Madini; Ongezeko la Thamani katika Sekta ya Madini; Maudhui ya Ndani katika Sekta ya Madini; Maendeleo ya Uchimbaji mdogo; Uboreshaji wa Utendaji na Maendeleo ya Rasilimali Watu; Idara, Mashirika ya Umma, Wakala, Programu na Miradi isiyo chini ya Wizara hii.
